DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 16, 2014

MWANAMUZIKI NA MUIGIZAJI NGULI DUNIANI RIHANNA AMETAJWA KUWA MKURUGENZI WA UBUNIFU WA PUMA

Kulikuwa na tetesi kuhusu Rihanna kusaini mkataba wa mamilioni na kampuni ya "Puma" lakini sasa imekuwa rasmi. Mwanadada huyo ameripotiwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Ubunifu kampuni ya Puma, kazi yake mpya ni kusimamia na kuangalia nguo na viatu vya kike vya michezo vya kampuni hiyo.

Rihanna "atafanya kazi na kampuni hiyo kuandaa na kutengeneza mitindo mipya katika bidhaa za Puma. Kampuni hiyo imesema
Riri ambae pia ni balozi wa kampuni hiyo, alisafiri mpaka Makao Makuu ya Puma yaliyopo Herzogenaurach, nchini Ujerumani kuwa na kipindi chake cha kwanza cha ubunifu pamoja na timu nzima ya wabunifu, kuchagua rangi, mitindo na kuweka mawazo yake kuhusu malengo na muelekeo wa sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment