DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 16, 2014

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA AJIUZULU


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu wadhifa wake kuanzia hii leo.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, iliyotolewa jana na Mkurugenzi wake, Salva Rweyemamu kwa vyombo vya habari imethibitisha kujiuzulu kwa Werema kuanzia jana. Alikuwa kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2009 alipochukua nafasi ya Johnson Mwanyika aliyestaafu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi la kujiuzulu kwa mwanasheria huyo.  

Pichani Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Jaji Frederick Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Sherehe ya kumwapisha Jaji Werema ilifanyika Ikulu jijini Dar tarehe Novemba  6, 2010 ikiwa ni siku chache baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani kwa awamu ya pili na kumteua tena kuendelea na wadhifa huo baada ya uteuzi wa awali wa 2009. Wapili kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na Katibu wa Baraza la Mawaziri. 




No comments:

Post a Comment