Kutoka
Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira
Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha 'The Mboni Show' uliofanyika
katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi
wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi
wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni
show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili
kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia Januari 02 mwaka 2015 siku ya Ijumaa saa 3 usiku hadi saa 4 usiku na marudio Jumanne saa 9:00 alasiri hadi saa 10:00 jioni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa
ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao, na kusema kuwa
amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia
watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna
kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimehamia
TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi, wote wazee na vijana na
hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki
ya jina hili”alisema Mboni.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw. Fadhili Chilumba
amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa (TBC)
na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama akina Mboni
na wanamkaribisha sana.
Nao
wadhamini wa Mboni Show, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF)
Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili
kuhamasisha, kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.
|
No comments:
Post a Comment