Watanzania
waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini
India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha
wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na
tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17
Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu
hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji
uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha
Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia
chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja
wa moyo na maini yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa
kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi
ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari
waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji
huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali
mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa
masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa
vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo
kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Hali
kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa
kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha.
Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive
Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa
kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini
yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne
kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”
Upasuaji
huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa
kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha
wengine wakiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama
Pygopagus, Ericana & Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa
kutenganishwa na wataalamu wa hospitali hiyo.
Matukio
amabayo yamepandisha chati na kuipa hadhi ya juu hospitali ya Apollo
iliyoko nchini India na nchi ya India kwa ujumla kama kiongozi katika
sekta ya afya na mfano wa kuigwa na nchi nyingine ikiwemo Tanzania.
Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya Tanzania ikitembelewa
idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana na ukosefu wa huduma
muhimu na za kisasa nchini. Wapacha walioungana hutambuliwa na kupewa
majina kutokana na jinsi muungano huo unapokuwa katika viungo mbali
mbali vya mwili.
Ikiwa
aina ya mapacha waliounganika wa Thoraco Omphalopagus ndio inayoongoza
kuripotiwa kwa asilimia 28% zaidi ya aina nyingine zote zinazotambulika
matukio mengi yakitokea zaidi Kusini-Magharibi mwa bara la Asia, Africa
and Brazili. Katika aina hii mapacha wanakuwa wameunganika kuaznia
kifuani mpaka chini ya kifua kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya
sehemu ya moyo, ini na baadhi ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula
(i).
Kulingana na hospitali ya Apollo kesi zinazohusu mapacha waliounganika
huwa ni nadra mathalan moja kati ya uzao 200,000 huonekana. Lakini,
asilimia 60 ya hao hufariki wakati asilimia 35 hufariki katika kipindi
kifupi baada ya kuzaliwa kutokana na sababu mbali mbali (ii).
Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na mafanikio, Dkt. Prathap C Reddy,
Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali za Apollo anasema, “Nikitazama
katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya watu tuliweza kuyagusa kwa
namna njema. Mbali na maumivu wanayopata watoto yatokanayo na ugonjwa,
wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko makubwa.
Nchi
nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala na hivyo
kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na kisasa.
Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika sikukuu hii ya Krismasi Jimmy
na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni binadamu wawili
tofauti.”
Chanzo:http://www.frankleonard.info |
No comments:
Post a Comment