DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, December 11, 2014

KAMPENI YA NYOTA YA KIJANI KANDA YA MAGHARIBI YAZINDULIWA TABORA

Baadhi ya wananchi wa wadau wa Afya wakiwa kwenye maandamano wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya NYOTA YA KIJANI uliofanyika eneo la kumbukumbu ya Mwl. Nyerere Tabora mjini.
Mmoja kati ya maafisa kutoka Wizara ya Afya Bi. Isabela Nyalusi akisoma taarifa fupi ya hali ya matumizi ya Uzazi wa Mpango kwa Kanda ya Magharibi ambapo inaonesha kuwa mikoa ya kanda ya magharibi ina kiwango kidogo cha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango (asilimia 19) ikilinganishwa na mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye asilimia 50.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dr. Fikiri Martine akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ambapo alieleza kuwa matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango yameanza kupanda katika siku za hivi karibuni licha ya kuwa bado jamii imekuwa ikikabiliwa na dhana potofu juu ya mpango huo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Bw. Suleiman Kumchaya akizungumza katika uzinduzi huo ambapo aliwataka wananchi mkoani Tabora kuzitumia njia za uzazi wa mpango kwa kuwa ni njia salama na zinazoweza kusaidia kupanga maisha katika mpangilio mzuri.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Bi. Kudra Mwinyimvua akizungumza katika uzinduzi huo ambapo aliwataka akina mama kujitokeza kutumia huduma za uzazi wa mpango.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Suleiman Kumchaya akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kampeni ya Nyota ya kijani, zoezi lililofanyika chini ya sanamu ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere mjini Tabora.


No comments:

Post a Comment