Menaja
wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto, akitoa
maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia)
ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika chumba cha
mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam , wa kwanza kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondoleo jijini Dar es
Salaam.
Serikali
imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao
(TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali. Akiongea
na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA),
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema
lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa ujumla
kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia mtandao. Balozi
Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi
kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote
zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili
kupunguza gharama. "Lengo kuu
la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii ili
kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na
pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi"
alisema. Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA),
Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa ikitekeleza majukumu
kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na
mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda sambamba na maendeleo ya
teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijamii
na kiserikali. "Wakala wa
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana mawasiliano baina ya
serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na Sekta binafsi
katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia utawala bora, anuai za
jamii, maswala ya afya na mazingira" alisema Sekondo Katika
Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi
ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo Sehumu ya Huduma za
Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za
maendeleo (TDCI). Mtandao wa
TaGLA,unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na wakala
wa serikali pamoja na sekta binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo ,
mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa nchini na nchi nyingine,
midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na mafunzo kwa njia
ya uongozi.
|
No comments:
Post a Comment