DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, December 16, 2014

DR SHEIN AONGOZA MKUTANO WA 8 WA BARAZA LA BIASHARA ZBC

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,  Nassor  Ahmed   Mazrui wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja kushiriki katika Mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) lililofanyika leo.
Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali  mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja kushiriki katika Mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) lililofanyika leo.
Rais Dk. Ali Mohamed Shein akiendesha mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) ulilofanyika leo kwenye Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Hassan Omar akijibu masuala mbalimbali yaliyoulizwa wakati wa Mkutano wa 8 wa  Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) mjini Unguja ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Mfanyabiashara Taufuk Salum Turky akichangia kuishauri Serikali kuchukua hatua za haraka katika kutoa maamuzi kwa miradi mbali mbali inayotaka kufunguliwa na wafanyabiashara wakati wa Mkutano wa 8 wa  Baraza la Biashara Zanzibar (ZBC) ulioendelea leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment