Sehemu
ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Akizungumza na
Waandishi na Habari mapema jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Hoteli ya Hayyat
Regency, Prof. Tibaijuka alisema kuwa udalali wake wa fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi
katika shule za Taasisi ya Barbo Johansson Girls Education Trust, na kwamba fedha aliyoipata ni shilingi Bilioni 1.66 ambazo zilitoka
katika kampuni ya James Rugemalira kama msaada kwa shule hiyo.
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi
ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James Rugemalira
ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi.
"Nikijiuzulu
hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani
fedha nilizopata ni za shule kwa ajili kukomboa elimu nchini hasa
kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za
shule’’alisema.
Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai
hata Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi alitoa shilingi milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.
Prof. Tibaijuka alifafanua kuwa
wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi
kufanya hivyo na kama angetaka fedha hizo angeweza kufuata hata katika shule na
kuchukua.
|
No comments:
Post a Comment