Aisha Mohammed
Mbegu 'Aisha Madinda' wakati wa Uhai wake.
Aliyekuwa
Mnenguaji na Muimbaji nguli wa Bendi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda amefariki
dunia jana Jijini Dar es salaam. Habari imethibitishwa na mmiliki
wa Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta, Asha Baraka. Mkurugenzi wa bendi hiyo alisema alipewa taarifa na Daktari mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala kuwa wameona kama
mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda
kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo
walipogundua kuwa ni yeye.
" Mimi
nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha
sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana
alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili
wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata
sielewi nini kimetokea" Alisema Asha Baraka.
Hata hivyo, taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa Madinda aliita
dereva wa Bajaj na kuomba apelekwe Hospitali ya Mwananyamala na ndipo alipokumbwa
na mauti akiwa njiani bila dereva huyo kujua mpaka alipofika hospitalini hapo.
Inaelezwa kuwa msiba wa Marehemu Aisha uko Kigamboni na huenda akazikwa leo huko huko.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina! |
No comments:
Post a Comment