Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Risasi Jumamosi: Unaweza kunipatia historia yako fupi ya sanaa tangu ulipoanzia mpaka sasa? Baba
Haji: Nilianza kuigiza 1998, nilianzia kundi lililoitwa Mtanzania
ambalo lilikuwa chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mwaka 2000 nikaenda
Nyota Academia kundi lililokuwa likiongozwa na mwalimu marehemu George
Otieno ‘Tyson’, mkurugenzi akiwa ni Singo Mtambalike ‘Richie’.
Sikuishia
hapo, mwaka 2002 tulianzisha Kundi la Kamanda Family nikiwa na Richie
Mtambalike ambapo tulicheza michezo mbalimbali kisha tukaamua kuanza
kucheza filamu ambapo tulicheza filamu ya Masaa 24 tukaona filamu ndiyo
mpango mzima.
Mwaka
2003 nilicheza filamu ya Miss Bongo niliyoshirikiana na Aunt Ezekiel,
iliyofuata ilikuwa ni Jeraha ya Ndoa, nilicheza na Monalisa. Mwaka 2004
nilikwenda Bukoba (Kagera) ambapo nilichukuliwa na Abantu Vision kwa
ajili ya kufanya sinema iliyohusiana na mambo ya HIV ilivyoingia
Tanzania. Filamu hiyo ilifanikiwa kuchukua Tuzo ya Ziff kama Filamu Bora
ya mwaka 2005.
Mwaka 2010 nilijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambapo nilisoma mpaka kumaliza mwaka 2013. Mwaka
2014 nilifanikiwa kucheza filamu nyingi kama vile Barbara, Kitoga,
Don’t Cry, Mary Mary, Charles Mvuvi, Mwandishi wa Habari, Jamila na Pete
ya Ajabu na Wa Mwisho Wewe.
Mwaka huu
ndiyo wa mavuno kwangu kwani nimejiandaa vema kutoa filamu zangu
mwenyewe ambazo zitakuwa na changamoto kubwa kwani nimesoma kwa ajili ya
kuja kuvifanyia kazi na kuibadili kabisa tasnia ya filamu. |
No comments:
Post a Comment