Alisema maandalizi ya Tamasha la Pasaka yamekamilika asilimia 90 na mwaka huu litakuwa la aina yake.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Msama, alisema mwaka huu
tamasha linaadhimisha miaka 15 tangu lianzishwe na wanatarajia kumwalika
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujumuika nao,
kwani ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati linaanzishwa.
Msama
aliwataja waimbaji wengine watakaokuwepo katika tamasha hilo kuwa ni
pamoja na John Lisu na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huku wakiwa
katika mazungumzo na mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Rose Muhando,
kutokana na maombi ya wapenzi wengi wa tamasha hilo. CHANZO: MJENGWABLOG
No comments:
Post a Comment