DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Saturday, March 21, 2015

ZITTO AFANYA MAAMUZI MAGUMU NA MAKINI, AACHIA NGAZI UBUNGE

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa Tiketi ya Chadema, Kabwe Zitto akisoma barua aliyomwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumtaarifu kuwa anang'atuka nafasi ya Ubunge. Pia aliwaaga Wabunge wenzake na kuahidi kurudi tena Mungu akijalia baada ya Uchaguzi wa mwaka huu.
Wabunge mbalimbali wakiwepo wa Chadema, Cuf, NCCR na CCM walionekana dhahiri kububujikwa na machozi kufuatia kujivua kwake Ubunge.

Mhe. Zitto Kabwe akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu mara baada ya kuwaaga Wabunge baada ya kuwasomea barua aliyomwandikia Mhe. Spika ya kung'atuka ubunge baada ya kuvuliwa Uanachama na chama chake cha CHADEMA.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni msemaji wa katiba na sheria wa kambi ya upinzani Bungeni Mhe. Tundu Lissu (wa pili kushoto) akiongea  na wabunge wenzake wakati akitoka katika kikao juzi jioni mara baada ya Zitto Kabwe kung'atuka Ubunge. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mhe. Engineer Christopher Chizza, Mhe. Mchungaji Peter Msigwa na Mhe. Ismail Aden Ragge.
Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka Bungeni mjini Dodoma juzi. Chini akiwa na Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe (kuhoto) na Mbunge mwingine.

No comments:

Post a Comment