Kutokana
na kubugia kiburudisho kupita kiasi, Shilole alishindwa kupanda boti
iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa bahari na hivyo kumpa kazi ya ziada
mchumba wake Nuh Mziwanda aliyelazimika kumrudisha garini ili warejee
nyumbani.
"Kusema
kweli mimi hata sielewi nilishindwaje kupanda boti, network ilikata,
nilishangaa tu kujikuta nipo kwenye bethidei ya Menina Mikocheni,
nafikiri kilichotokea muulize baby wangu Nuh Mziwanda," alisema Shilole
baada ya kuulizwa kuhusu 'kuzimika' kwake.
Nuh
Mziwanda alikiri kuwa mpenzi wake alipoteza fahamu, kiasi cha
kumlazimisha yeye kumbeba na kumrudisha tena klabu ya Paparazi ambako
alipatiwa maji baridi kwa wingi huku akipigwa na kiyoyozi cha nguvu
kabla ya kwenda kwenye shughuli ya Menina. CHANZO: GLOBAL PUBLISHER |
No comments:
Post a Comment