Ndege ya shirika la ndege la Germanwings.
Ndege ya abiria inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.
Ndege
hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya
nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.
Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.
Ndege
hiyo ya Ujerumani ilianguka katika eneo lisilo na majengo ambalo
halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.
Hali ya
hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha
kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.
Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .
|
No comments:
Post a Comment