Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu Dar es Salaam
Mtangazaji wa Clouds FM, Millard
Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu wamesifia gari jipya la
Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na kusambazwa na kampuni ya
Diamond Motors (Hansa Group).
Katika uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya
Diamond Motors wauzaji pekee wa magari kutoka Mitsubishi waliwaalika
Millard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya Mitsubishi ASX
kabla ya uzinduzi.
Mastaa hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo
vya kisasa juu vyenye mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia
mwonekano wa pande zote.
Meneja mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo
lenye luninga ndogo inayocheza DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka
vyanzo mbalimbali ni maalumu kwa vijana wa kisasa na familia kwani
Mitsubish ASX limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe
na nguvu ya 150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa
mwendokasi mkubwa na kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo.
“ASX ni mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama kama
Pajero ambayo tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania
magari imara na yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra.
ASX toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara
likiwa na bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo
kumfanya mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.
“ASX kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu kukidhi mazingira
ya Tanzania hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote dereva wa
kawaida anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara zenye
makorongo” alisema Ganatra
Injini ya gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III
CVT inayoisaidia mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na
uimara wa usukani unaosaidia mikono ya dereva kuwa salama hata anapokuwa
katika mwendo mkali.
Hansa Group inayofanya biashara kama Diamond Motors Limited,
imekuwa ikifanya kazi ya katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 1980,
ikitoa huduma kwa wasambazaji na wadau wa usafiri.Kampuni hiyo huhusika
na bidhaa/ huduma mbalimabali. Shughuli za Hansa Group zimesambaa karibu
nchi zote za jumuia ya Africa ikitoa huduma kama vile za uchimbaji,
Umeme, Mafuta na Gesi, Reli,Ulinzi, Ujenzi, Usafiri, kimataifa na
jumuhia za kimataifa.
|
No comments:
Post a Comment