DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Tuesday, March 24, 2015

KINANA AWASILI MOSHI VIJIJINI KWA KISHINDO, APOKELEWA NA FARASI

Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukipokelewa kwa farasi wakati alipowasili katika kijiji cha Mikocheni TPC wakati alipoanza ziara yake ya kukagua na kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM katika jimbo la Moshi Vijijini akitokea jimbo la hai ambapo alimaliza ziara kama hiyo jana, Kinana akiwa katika jimbo la Moshi vijijini atashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na wananchi na kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM jimboni humo akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MOSHI VIJIJINI- KILIMANJARO)

Farasi wakiongoza msafara huo ulipowasili kijiji cha Mikocheni TPC Moshi vjijini.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika kijiji cha Mikocheni TPC, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Dk Cyril Chami.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Kilimanjaro Mh. Betty Machangu.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na wananchi mara baada ya kupokelewa.
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea eneo la mkutano ambapo amezunguza na wananchi baada ya mapokezi.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Dr. Cyril Chami akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mikocheni.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akwasalimia wananchi katika kijiji cha Mikochenzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliofurika kumpokea katika kijiji cha Mikocheni jimbo la Moshi Vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aki akiwasili katika ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki mkutano wa wajumbe wa halmashauri kuu ya Moshi vijijini, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na kushoto ni Iddi Juma Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro. 
Msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma wakati alipowasili katika ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akishiriki kupiga ngoma wakati msafara wa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment