Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani mjini London.
Marekani
na washirika wake watatu barani Ulaya wameapa Jumamosi (21.03.2015) kuendelea na mazungumzo na Iran kuhusiana na mpango wa nchi
hiyo wa kinyuklia licha ya tofauti zilizopo wakati muda wa mwisho
ukikaribia.
"Tuko
katika hatua muhimu katika majadiliano," Waziri wa Mambo ya Kigeni wa
Marekani John Kerry na wenzake kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na
Umoja wa Ulaya wamesema katika taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo
katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London.
"Iwapo
tutaweza kutatua masuala yote makubwa, kazi ya kiufundi itafuatia
kubadilisha mpango elekezi kwa waraka wenye maelekezo." Kerry amesema
mazungumzo mjini London yalikuwa "yenye matunda" na yanaonesha kuwa
mawaziri wako pamoja katika haja ya kupatikana makubaliano sahihi, na
sio tu makubaliano yoyote."
Iran
yatakiwa kuchukua uamuzi mgumu iwapo makubaliano yatapatikana , maelezo
kamili ya makubaliano yanatarajiwa kufikiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi
Juni, 2015. Kerry na mawaziri wengine wa mambo ya kigeni mjini London wamesema
Iran inahitajika "kuchukua uamuzi mgumu" kabla ya kupatikana
makubaliano kamili. "Suluhisho lolote linapaswa kuwa pana, la muda
mrefu na linaloweza kuthibitika," wamesema. "Tumekubaliana kwamba
kumekuwa na hatua zilizopigwa katika maeneo muhimu licha ya kuwa bado
kuna masuala muhimu ambayo hayajafikiwa makubaliano.
"
Akizungumza mapema jana Jumamosi (21.03.2015) katika mji wa Lausanne
nchini Uswisi, Kerry amesema licha ya kwamba "tofauti muhimu bado zipo"
na Iran pande hizo mbili zina "fursa ya kujaribu kufikia makubaliano"
katika muda wa siku kumi zijazo.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius, wakati huo huo, amesisitiza
kwamba makubaliano kamili ni lazima yafikiwe pamoja na Iran. Ni muhimu
kufikia makubaliano ambayo mataifa yote ya kimkoa kama vile Uturuki na
Saudi Arabia, yanaweza kuyaamini, ameiambia radio ya Ufaransa Europe 1,
na kuongeza kwamba Iran yenye silaha za kinyuklia itaanzisha mashindano
yenye mwelekeo mbaya ya kinyuklia katika Mashariki ya Kati. Gerard
Araud , Balozi wa Ufaransa nchini Marekani, amesema siku ya Ijumaa
(20.03.2015) kwamba msisitizo wa Marekani juu ya muda wa mwisho wa
tarehe 31 Machi ni, "mbinu mbovu" ambayo inaweka "mbinyo kwetu kufikia
makubaliano ya aina yoyote kwa gharama yoyote.
Iran
yasema Marekani inaonesha "ubabe" Iran imeonesha hali mchanganyiko jana
Jumamosi (21.03.2015) wakati kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei
alipoishutumu Marekani kwa kufanya "ubabe" na amesisitiza kwamba vikwazo
ni lazima viondolewe kabla ya kufikia makubaliano. Amesema kuwa,
Marekani inasema "tutie saini makubaliano na watafanya uchunguzi kuhusu
tabia yetu katika makubaliano hayo na baadaye wataondoa vikwazo," Televisheni ya Iran ya Press imemnukuu Khamenei akisema.
"Haya ni
makosa na hayakubaliki na Iran haitakubali hilo," Khamenei amenukuliwa
akisema. Wakati Marekani iko tayari kuondoa sehemu ya vikwazo vya
kiuchumi haraka, hakuna nia ya kuondoa haraka vikwazo vilivyowekwa na
baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vinavyopiga marufuku mauzo
yanayohusiano na nyuklia nchini Iran, wamesema maafisa wa Marekani.
Rais
Hassan Rowhani amesema Iran ina nia thabiti katika mazungumzo hayo na
"kufikia makubaliano ya mwisho ni jambo linalowezekana," wakati Waziri
wa Mambo ya Kigeni Javad Zarif amenukuliwa akisema majadiliano yamepiga
hatua muhimu" wiki hii.
MWANDISHI: SEKIONE KITOJO/DPAE/RTRE-DW.
|
No comments:
Post a Comment