Mbunge
wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda
na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area
'D' mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za
chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya
Urais 2015.
Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.
Aidha,
na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao
vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari
la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki
katika uchaguzi kwa kupiga kura.
|
No comments:
Post a Comment