RIAS Mstaafu wa awamu ya pili Ali
Hassan Mwinyi ameombwa kuhudhuria kwa mara nyingine katika Tamasha la
Pasaka linaloadhimisha miaka 15 mwaka huu.
Mwinyi ndiye mgeni muasisi wa tamasha hilo ambako kwa mara ya kwanza alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la mwaka 2000.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama anapenda rais huyo mstaafu
ahudhurie siku hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi muasisi
ambaye pia ni mlezi, hivyo akihudhuria atajionea maendeleo yake.
“Nitapenda sana iwapo rais Mwinyi
atahudhuria siku ya Tamasha ili aweze kushuhudia muendelezo wa Tamasha
tangu alipolizindua mwaka 2000,” alisema Msama.
Alisema hadi sasa maandalizi
yamekamilika hivyo mashabiki wa nyimbo za injili wakae mkao wa kula
wakisubiria tamasha hilo mapema mwanzoni mwa mwezi ujao.
“Mashabiki wakae tayari maandalizi
yamekamilika, tunachosubiri ni siku yenyewe ifike, waimbaji maarufu
watakuwepo wakisufu na kuabudu, hivyo ni wakati wenu mzuri wa kwenda
kupata neno la Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema.
Tamasha hilo la kimataifa
litakalobeba waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ndani na nje ya
nchi litafanyika mwezi ujao Dar es salaam na baadae kwenda katika baadhi
ya mikoa.
Waimbaji watakaohudhuria Tamasha
hilo ni pamoja na Jessica Honore, Joshua Mlelwa, Upendo Nkone, Kwaya ya
Kijitonyama na John Lisu.
Kwa upande na waimbaji kutoka je
ya Tanzania atakuwepo Rebecca Malope na Solly Mahlangu (Afrika Kusini),
Faustin Munishi (Kenya).
|
No comments:
Post a Comment