DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Monday, March 23, 2015

WILAYA YA MLELE YATUMIA SHILINGI 2.138 BILIONI KATIKA MIRADI YA MAJI KWENYE KATA TANO ZA WILAYA HIYO

Na Kibada Ernest-Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imetumia kiasi cha shilingi 2.138 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika  kata tano zilizoko kwenye Halamshauri hiyo ambazo ni fedha za wafadhili kupitia miradi ya benki ya dunia.
Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Mlele Gration Kato alieleza kuwa miradi hiyo imejengwa kwa ufadhili wa benki ya dunia na imetekelezwa kwenye vijiji vya Kibaoni Kata ya Kibaoni  kwa thamani ya shilingi  289 milioni,Kijiji cha  Mbede  Kata ya Mbede mradi wenye thamani ya shilingi 334 milioni.
Miradi mingine imetekelezwa kwenye Kijiji cha Usevya kwa thamnai ya shilingi 441 milioni, mradi wa maji katika Kijiji cha Kibaoni uliotekelezwa kwa thamani ya shilingi  548 milioni, pamoja na mradi wenye thamani ya shilingi 526.8 milioni hivyo kufanya jumla ya miradi yote kutekelezwa kwa gharama ya shilingi 2.138, bilioni.
Akizungumzia kuhusu mradi wa maji katika Kijiji cha Mirumba alieleza kuwa wanatarajia kuendela na ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho kwa gharama ya shilingi 700 milioni.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa Halmshauri ya Mlele inajumla ya wakazi wapatao 138,323 kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kati ya watu hao ni asilimia 42,tu ya watu wanaopata maji safi na salama sawa na watu 58,095.
Akaongeza kuwa kwa mwaka  2014  wakati wa kuazimisha wiki ya maji  watu  waliokuwa wanapata maji safi na salama walikuwa asilimia 39.ambapo kwa mwaka 2015 wanaopata maji safi na salama ni asilimia 42,na wameweka lengo ifikapo mwaka 2016/2017 wafikie asilimia 67 ya watu wanaopata maji safi na salama katika wilaya ya hiyo.
Akizungumzia mikakati ya kupambana na tatizo la upatikanaji wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele,Wilaya imeagiza mtambo mdogo wa kuchimba visima virefu kwa fedha za mapato ya ndani,pia Halmashauri inajenga ofisi za watumiaji maji katika Kanda za Mamba,Mbede na Usevya.
Lengo la kujenga ofisi hizo ni kurahisisha uendeshaji na matengenezo ya miradi ya yote iliyojengwa ili iwe endelevu na wananchi waweze kuihimili na kuendesha wenyewe,Kauli mbiu ya maazimisho ya wiki ya maji mwaka huu ni maji kwa maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment