Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi(kulia) na Benjamin
William Mkapa(kushoto) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea
Kutako jijini Windhoek Namibia leo.Viongozi hao walihudhuria sherehe za
maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia ambapo pia Rais wa awamu ya
tatu wa Namibia Dkt.Hage Geingob aliapishwa katika uwanja wa
Independence jijini Windhoek.Chama cha ukombozi cha Namibia SWAPO
kilizaliwa nchini Tanzania na kuendesha harakati za ukombozi mpaka mwaka
1990 ambapo nchi hiyo ilipata uhuru.
(picha na Freddy Maro).
|
No comments:
Post a Comment