DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, March 22, 2015

WAZIRI MEMBE: MAGARI YA KITALII YA TANZANIA RUKSA KUINGIA UWANJA WA JOMO KENYATTA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kati ya  Serikali za Tanzania na Kenya juu ya kuruhusu tena magari ya kitalii ya Tanzania kuingia Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na kurudisha idadi ya awali ya safari za ndege za Kenya ambazo ni 42. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Rajabu Gamaha (kushoto) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Membe.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatlia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Waandhishi wa Habari. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Bibi Rosemary Jairo, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine,  Bw. Innocent Shiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia mazungumzo ya Waziri Membe na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani. (Picha na Reginald Philip)

No comments:

Post a Comment