Jeremy Mathieu akipiga mpira wa kichwa uliozaa bao la kwanza kwa Barcelona.
MABAO
mawili yaliyofungwa na Jeremy Mathieu katika dakika ya 19 na Luis Suarez
dakika ya 56 yameipa ushindi timu ya Barcelona dhidi ya mahasimu wao
Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani Nou Camp usiku huu.
Katika mtanange huo wa La Liga, Barcelona wametoka kifua mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Bao la Real Madrid limewekwa kimiani na Cristiano Ronaldo dakika ya 31 ya mchezo. Kwa matokeo hayo, Barcelona wamefikisha pointi 68 mbele ya Real Madrid wenye pointi 64. |
No comments:
Post a Comment