"Kama
mimi ni mwizi na tapeli, hivi hata usalama wanashindwa kuwaeleza ukweli
washughulike na mimi? Ndiyo maana watu tuliowafukuza Chadema
wamewapokea eti wamehama chama. Wameingizwa mjini hao," Lema
Siku moja
baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwapokea viongozi
wawili akisema wanatoka Chadema na kumtuhumu Mbunge wa Arusha, Godbless
Lema kuwa anatumia madaraka yake kujinufaisha na mali za umma, mbunge
huyo amejibu akisema: "Kinana amepigwa changa la macho."
Akiwa
Arusha mwishoni mwa wiki Kinana aliwapokea waliokuwa wenyeviti wa
Chadema katika Wilaya ya Monduli, Amani Silanga na wa Ngorongoro,
Revocatus Palapala lakini jana Lema alisema viongozi hao
walikwishatimuliwa Chadema tangu mwaka 2013.
Kinana
alisema migogoro ya CCM ndiyo iliyokinufaisha Chadema na Lema akaingia
madarakani, lakini akawataka wananchi kujutia uamuzi huo na kutorudia
kumchagua mbunge huyo.(P.T)
"Mbunge
wenu ameshindwa kutekeleza kile mlichomtuma bungeni badala yake anatumia
madaraka yake kujimilikisha mali za umma na kutukana hovyo," alisema na
kuongeza:
"Mfano ni
lile shamba alilopewa na Mayala ambalo ameliuza, trekta na vifaa
vingine vyote ameviuza lakini migogoro ya ardhi na maji ameshindwa
kuitatua."
Majibu ya Lema
Akijibu
tuhuma hizo, Lema alisema Kinana amepigwa 'changa la macho' na
amefanyiwa maigizo kama ya futuhi na watu wa usalama wameshindwa
kumwambia ukweli.
Alisema mambo yote aliyoambiwa ni uongo mtupu ambao yeye hawezi kusumbuka nao.
"Kama
mimi ni mwizi na tapeli, hivi hata usalama wanashindwa kuwaeleza ukweli
washughulike na mimi? Ndiyo maana watu tuliowafukuza Chadema wamewapokea
eti wamehama chama. Wameingizwa mjini hao," alisema.
Alisema:
"Silanga na Palapala walifukuzwa tangu Novemba 30, 2013 baada ya
kubainika kuwa kwenye mtandao wa Zitto na wote walitimkia ACT kama
walivyofanya kina Mwigamba (Samson) na Kitila Mkumbo," alisema Lema
akitoa nakala ya taarifa kwa vyombo vya habari.
Alisema
baadaye Silanga na Palapala walijiunga CCM na Palapala aligombea na
kushinda uenyekiti wa Kijiji cha Wasso wilayani Ngorongoro kwenye
uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba 14, mwaka jana.
"Ni
maajabu ya mwaka mwenyekiti wa kijiji kupitia CCM tangu Desemba 14,
mwaja jana, apokewe na Kinana akitangazwa kukihama Chadema?" alisema
Lema.
|
No comments:
Post a Comment