DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, March 22, 2015

MH. ZITTO KABWE SASA NI MWANACHAMA HALALI WA CHAMA CHA ACT-TANZANIA

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya yenye namba 007184 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni
Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda.
***********
Chama cha ACT-Tanzania leo kimemtangaza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe kuwa mwanachama mpya wa chama hicho kuanzia.

Zitto amesema ameamua kujiunga na chama hicho kwa kuwa ni chama chenye misingi bora ya uongozi na hivyo yeye kama kiongozi ameamua kwenda huko kwani anaamini kuwa Chama hicho ndicho kitakacholeta mapinduzi ya kweli kwenye siasa.

Mbali na Mh. Zitto Kabwe,wengine waliojiunga na chama hivyo ni pamoja na hao waliopo kwenye orodha hiyo hapo chini.
Orodha ya waliojiunga na Chama cha ACT-Tanzania leo.
Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda akionyesha kipeperushi cha Chama chao mbele ya waandishi wa habari wakati wa kumtangaza mwanachama wao mpya ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe.
Aliekuwa Mbunge  wa Jimbo Khamisma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe akinzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na Chama cha ACT-Tanzania,katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam.Kushoto ni
Mwenyekiti wa Tawi la Tegeta wa Chama cha ACT-Tanzania,Lugano Mwaikenda.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Selemani Msindi "Afande Selle" akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kuungana na Mh. Zitto Kabwe kujiunga na chama ACT-Tanzania kutokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba na kushoto ni rafiki wa Afande Selle ambaye nae amejiunga na Chama hicho,Adam Shanzy.
Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania, Samson Mwigamba akimkabishi kadi ya uwanachama,Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Selemani Msindi "Afande Selle" ambaye amejiunga na chama hicho akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Sehemu ya Wanachama wa Chama ACT-Tanzania wakionyesha mabango ya kumkaribisha Mwanachama mwenzao ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe.
Katibu Mkuu wa Chama ACT-Tanzania,Samson Mwigamba pamoja na Zitto Kabwe wakinukuu kwenye makaratasi maswali mbali mbali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano wao uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena,Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment