Hajji Manara (kulia) akiongea na waandishi wa habari, kushoto ni katibu mkuu wa Simba SC, Stephen Ally
AFISA habari mpya wa klabu ya
Simba, Hajji Manara ametambulishwa rasmi na uongozi wa klabu hiyo katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo,
Mtaa wa Msimbazi Kariaokoo, Dar es salaam.
Hajji anarithi kiti cha Humphrey Nyasio aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.
Mara
baada ya kutambulishwa na Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally, Hajji,
mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Sunday Manara ameishukuru klabu
yake kumteua yeye tena akiwa mlemavu wa ngozi ‘Albino’, huku wenzake
wanaendelea kuchinjwa nchini na akasema Simba ndio wapiganaji wa kweli.
Manara baada ya kutangazwa
na yeye ametangaza utaratibu mpya wa idara yake akisema kila Ijumaa
watakuwa na mkutano na waandishi wa habari, lakini kocha wao atazungumza
na waandishi mara moja kwa mwezi na yeye hatakuwa anaongea mambo ya
ufundi.
Katika mkutano huo, Katibu Mkuu, Stephen amefafanua suala la mshambuliaji wao, raia wa Uganda,
Danny Sserunkuma kuwa aliondoka kwa ruhusa yao akiuguliwa na mkewe Kenya
na leo (jana) anarejea.
Katibu huyo alisema sio kweli
kwamba aliondoka kwa kuhusishwa katika ushirikina taarifa ambazo hata
mwenyewe Sserunkuma alizikanusha. CHANZO: SHAFFIHDAUDA.CO.TZ
|
No comments:
Post a Comment