DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, March 22, 2015

ZITTO ATUA RASMI ACT, APEWA KADI YENYE NAMBA 007194, KUONGEA NA WANAHABARI LEO

Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
HAYAWI hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Zitto akionyesha kadi yake kwa wanachama wa ACT.

Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho jana.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao Makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
HAYAWI hayawi… Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
CHANZO: Modewji Blog

No comments:

Post a Comment