Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania mstaafu . Jenerari Mrisho Sarakikya
akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati
alipokutana naye baada ya kutembelea kata ya Sing'isi na kusaslimiana na
wananchi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha yenye lengo la
Kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayotekelezwa na
serikali kwa pamoja na wananchi huku akihamasisha uhai wa chama cha
Mapinduzi , Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi.
Naye Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia katika Mkutano wa
hadhara uliofanyika kata ya Mbunguni amewaambia wananchi katika mkutano
huo amemshutumu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kwa
kutosikiliza ushauri alioutoa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwa wilayani Loliondo na Ngorongoro kwa mawaziri
ambao wizara zao zinahusika moja kwa moja katika maamuzi na
kushughulikia matatizo ya migogoro ya Ardhi mkoani Arusha ambapo
kumekuwa na migogoro karibu wilaya zote, kati ya mbuga za wanyama na
vijiji ama kati ya vijiji na vijiji.(P.T)
Nape
amesema wakati waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William
Lukuvi akiitikia na kupokea ushauri huo na kuhamishia shughuli zake
mkoani Arusha ambapo kwa sasa yuko mkoani humo akikutana na viongozi
mbalimbali pamoja na wananchi ili kutatua migogoro hiyo, Nyalandu amekaa
kimya anaendelea na mambo yake.
CCM ndiyo
yenye mkataba na wananchi kwani ndiyo iliyoomba kura kwa wananchi na Mh
Waziri Nyalandu ana mkataba na CCM ambayo imempa kazi ili afanye kazi
na kutatua matatizo ya wananchi, CCM haiwezi kukubali mambo yaiharibike
kwa watendaji wa serikali kutowajibika kwa wananchi kwani ndiyo
itakayoadhibiwa na wananchi wakati wa uchaguzi ujao, "Hivyo Nyalandu
anatakiwa kufanya kazi ambayo CCM imempa na si kutafuta watu wa kumtetea
si sawa" Amesema Nape Nnauye. |
No comments:
Post a Comment