Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisikiliza risala ya umoja wa
wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga iliyokuwa ikisomwa kwake na
Mwenyekiti wa umoja huo Ndugu Willington Kiziba Ndyetabura (Kulia).
Katika risala hiyo yalikuwepo malalamiko mbalimbali ikiwemo ya matumizi
ya mashine za EFD ambapo ni pamoja na gharama kubwa za mataengenezo, Ada
ya ukaguzi wa majanga ya moto (Fire), Kupanda mara mbili kwa
kodi ya mapato kwa wafanyabiashara wadogo na Ulinzi na Usalama kwa
wafanyabiashara. Wafanyabiashara hao walihoji ni vigezo gani
vilivyotumika kupandishwa kwa kodi hiyo.
No comments:
Post a Comment