Rais
Obama amemtumia salaam za pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin
Netanyahu kutokana na ushindi uliokipata chama chake katika uchaguzi
uliofanyika Jumanne.
Lakini
Bwana Obama ameelezea dhamira yake ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya
Israel na Wapalestina kuwa ni kuunda taifa la Palestina.
Awali
Ikulu ya Marekani ilielezea wasiwasi kuhusu ahadi ya Bwana Netanyahu
wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba asingeruhusu kuundwa kwa taifa la
Palestina.
Waziri
mkuu wa Israel tangu wakati huo amelegeza msimamo wake, akisema
atakubali suluhisho la kuwepo mataifa mawili jirani endapo usalama
katika eneo la Mashariki ya Kati utaimarishwa.BBC |
No comments:
Post a Comment