Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh
Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Chadema wamekosoa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kupata hati zenye mashaka na kueleza
kuwa hesabu za vyama vyao zipo sahihi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape
Nnauye na Mkurugenzi wa Fedha wa Chadema, Anthony Komu walidai taarifa
ya CAG ndiyo yenye upungufu.
Nape
katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari yaliyorushwa moja kwa
moja na kituo cha Radio 5 Arusha alisema, kuna tatizo la kutokubaliana
kutokana na ukaguzi wa CAG.
Alisema
mahesabu ya CCM yanayotokana na fedha za ruzuku kutoka serikalini yapo
sahihi lakini wana mgogoro na CAG ambaye anataka mahesabu juu ya mali
zote za CCM."CCM ina miradi mingi kwa mfano hapa Arusha tuna uwanja wa
Sheikh Amri Abeid awali uwanja huu, ulikuwa unasimamiwa na Mkoa wa
Arusha pekee, sasa mkoa umegawanywa siyo rahisi kuwa na mahesabu yote,"
alisema.(P.T)
Alisema
kwa maagizo ya CAG, kuandaa hesabu na taarifa za mali zote za CCM,
inahitaji kutumika kwa zaidi ya Sh1 bilioni jambo ambalo ni gumu.
"Sisi
tunadhani CAG anapaswa kukagua mahesabu ya fedha za ruzuku tunazopewa na
Serikali lakini siyo mahesabu ya mali zote za CCM," alisema.
Kwa
mujibu wa taarifa ya CAG, ameainisha vigezo saba tofauti
vilivyosababisha hesabu za CCM kupata hati yenye mashaka na kueleza kuwa
CCM imekosa uhalali wa kisheria kumiliki baadhi ya mali ilizonazo.
Ukaguzi
huo wa CAG umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya
Vyama vya Siasa, iliyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 7 ya mwaka
2009, inayompa CAG mamlaka ya kukagua hesabu za vyama vya siasa.
Ilibainisha
vigezo vingine vya hati yenye mashaka kuwa ni CCM kutowasilisha taarifa
ya mapato yake ya fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali zilizofikia
Sh1,526,536,802, huku CAG pia akishindwa kupata nyaraka za kuthibitisha
matumizi na malipo yaliyofanywa na chama hicho yanayofikia
Sh6,045,438,052.
Kwa
upande wa Chadema, Komu alisema ripoti ya CAG ina upungufu kwani,
inataka chama hicho kuandaa taarifa za mahesabu na uthamini wa mali hadi
mikoani.
"Mapungufu
(upungufu) ambayo alianisha ya kutofanya uthamini wa mali zetu kutokuwa
na mahesabu ya benki katika ngazi mbalimbali na vitabu vya risiti kwa
baadhi ya maeneo ni mambo ambayo huwezi kuyakamilisha kutokana na mfumo
wa vyama vyetu," alisema.
Alikiri kuwa chama kuwa na akaunti nyingi kwa madai kuwa kila mkoa, wilaya na jimbo wana akauti yao. CHANZO: MWANANCHI.
|
No comments:
Post a Comment