Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo. Na Dotto Mwaibale
WIZARA ya Nishati na Madini
imetangaza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania kwa ufadhili wa
Serikali ya Watu wa China kwa kipindi cha mwaka 2015.
Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masoud Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wanahabari.
Alisema nafasi hizo za masomo ni
ngazi ya Shahada ya Juu ya Uzamili katika fani ya gesi katika Chuo
Kikuu cha Jiosayansi cha China ambapo muda wa kutuma maombi hayo
umeongezewa hadi kufikia Machi 30 mwaka huu.
Alisema waombaji wa ufadhili huo
wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Ardhi au Uhandisi kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na serikali, na muombaji awe na miaka kati ya 35 na 40.
Katika hatua nyingine Masoud alisema mitambo ya kuchakata gesi imekamilika kwa asilimia 96.
Alisema kukamilika kwa mitambo
hiyo inamanufaa makubwa ikiwemo umeme wa uhakika na gharama nafuu kwani
utekelezaji wa mradi huo utaliwezesha taifa kuokoa trilioni 1.6 kwa
mwaka zinazotumika kununua mafuta kwa ajili yua kuzalisha umeme.
Masoud alisema kukamilika kwa
mradi huu kutachochea maendeleo ya viwanda nchini kwani viwanda vingi
vimeonyesha nia ya kutumia nishati ya gesi asilimia katika kuendesha
mitambo yake ya uzalishaji.aidha umeme wa uhakika utapunguza gharama
za uzalishaji na kufanya bidhaa za tanzania kukuzika katika masoko
mbalimbali duniani.
Alisema tatizo la ajira nalo
litapungua kutokana na kukamilika kwa mradi huu ambao utapelekea ajira
mpya nyingi kupatikana na kutokana na kuwepo kwa umeme wa kutosha na
uhakika katika viwanda ambapo viwanda vingi vitaanzishwa vilevile
umeme utakwenda mashambani na kwenye biashara nyingine hivyo kwa namna
moja ama nyingine ajira zitaongezeka.
Alisema gesi hiyo asilia pia
hutumika kama malighafi katika viwanda mbalimbali kama,mbolea,
kemikali,aluminiamu pamoja na kutengeneza vifaa vya plastiki uanzishaji
wa viwanda vipya kutokana na matumizi ya gesi asilimia kutachochea .
kukua kwa uchumi wa nchi yetu na kwa upatikanaji wa ajira mpya nyingi kwa vijana wetu.
Aliongeza kuwa Serikali kupitia
wizara hiyo chini ya Mradi Endelevu wa Usimamizi wa Rasilimali Madini
(SMMRP), inakaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya pili kwa wachimbaji
wadogo nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com) | |
No comments:
Post a Comment