"Na mimi ni mhanga katika jambo hili kwa sababu watu wanaishi kwa mashaka, hivyo naomba hukumu za wahalifu hao ziwe wazi kila mtu aone ili iwe fundisho kwa waliofanya na wale wanaofikiria siku moja wajiingize kwenye unyama huo.
"Pia naomba sheria za mauaji zirekebishwe ili kulinda haki za walemavu mara baada ya kufanyiwa unyama sambamba na kuwapa adhabu kali wale wote wanaokutwa na hatia dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi," alisema Kweigyir.
Kweigyir ni miongoni mwa wabunge wanaopigania haki za kuishi za watu wenye ulemavu wa ngozi, likiwa
ni janga lililoshika kasi katika maeneo kadhaa ya Tanzania, hususan katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kunakoonekana kushamiri vitendo vya kuwadhuru na kuwaua walemavu hao wa ngozi.
No comments:
Post a Comment