Hali ya hewa katika Milima ya Alps nchini Ufaransa
Siku ya jana ndege ya Ujerumani
ilianguka katika eneo la milima ya Alps huko Ufaransa na kuua watu wote
wapatao mia moja na hamsini waliokuwemo.
Waathirika wa ajali hiyo wanatoka nchi
mbali mbali ambapo arobaini na tano ni wahispania huku zaidi ya sitini
wakiwa ni wajerumani.
Kumi na sita, kati yao walikuwa ni
wanafunzi kutoka shule moja nchini Ujerumani ambao walikuwa wakijerea
kutoka katika ziara ya kutembelea Hispania.
Pierre-Henry Brandet msemaji wa Wizara
ya Mambo ya ndani amewaambia waandishi wa habari kwa zoezi la kuuopoa
na kutambua miiili ndio kinachoopewa kipau mbele.
"Kipaumbele chetu ni kupata miili
mingi kwa kadri tuwezevyo ili kuwafanya wataalam wa utambuzi wa uhalifu
waweze kuifanyia utambuzi.
Na sio miili pekee kitu chochote
ambacho kitatusaidia kuitambua miili kama vile mizigo ya abiria ambayo
atakuwa ameibeba itachukuliwa na itatuwezesha
kuupeleka mwili katika nchi aliyotoka lakini ni mapema kusema ni wakati gani."
Naye Raisi wa Marekani Barack Obama
amesema kwamba taifa lake linaungana na mataifa ya Ujerumani na Hispania
katika kipindi hiki kigumu walichopoteza
wapendwa wao."Nataka kusema kwamba
mawazo na sala zetu tunazielekeza kwa marafiki zetu walioko Ulaya ,na
hasa kwa watu wa nchi za Ujerumani na
Hispania ,kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyotokea nchini Ufaransa.
Inaumiza kwa sababu ajali hiyo
imepoteza watoto wengi kwa wakati mmoja ,na walio wengi watoto
wachanga.nilimpigia simu kansela wa Ujerumani Angela
Merkel natarajia kuongea na Raisi ama
waziri mkuu wa Hispania Rajoy baadaye leo kutoa salamu za rambi rambi
kutoka kwa watu wa Marekani ,lakini pia
kutoa msaada wowote utakao hitajika wakati huu wa uchunguzi wa chanzo cha ajali iliyosababisha janga kubwa.."BBC. |
No comments:
Post a Comment