Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano hilo wakisikiliza mada zilizokuwa zinazungumzwa.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Viti Maalum ambaye pia ni mlemavu wa ngozi (albino), Al -Shaimaa Kweigyir, amekemea vikali
unyanyapaa unaofanywa na baadhi ya Watanzania juu ya jamii yenye ulemavu
wa ngozi na kusema kwamba inawafanya watu hao waishi kwa unyonge.
Mbunge
huyo aliyasema hayo jana katika kongamano la kujadili nini kifanyike
ili kutokomeza mauaji na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa walemavu wa
ngozi llilofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki
na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wanazuoni.
“Wapo
watoto wanaozaliwa katika hali ya albino ambao wamekuwa wakiishi kwa
mashaka makubwa kutokana na unyanyapaa dhidi ya jamii nyingine ambayo
ukiangalia kwa kina hakuna tofauti yoyote kati ya albino na wengineo.
“Naomba
jamii ione albino ni watu kama wao kwa kuhakikisha kwamba
wanawathamini, wanawajali na kuwalinda wakati wote, huku wakianzia
kwenye uondoaji wa fikra mgando na unyanyapaa wanaofanya kwa baadhi ya
kaya,” alisema.
Mbunge Shaimar ni miongoni mwa viongoz wa serikali waliojiweka busy
katika kutafuta mbinu za kuweza kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi albino yanayoendelea kutokea katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania. CHANZO: HAKINGOWI.COM
|
No comments:
Post a Comment