MABINGWA
mara ya 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wamevunja
mwiko wa Mgambo JKT kutofungwa na vigogo Simba, Yanga kwa misimu mitatu
katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga baada ya kuifumua mabao 2-0 katika
mechi ya ligi kuu iliyochezwa jana jioni.
Mabao ya
Yanga yamefungwa kipindi cha pili na winga mwenye kasi Saimon Msuva na
mtaalamu wa magoli ya kichwa na mfungaji bora msimu uliopita, Amissi
Tambwe.
Bao la leo ni la 9 kwa Msuva na la 5 kwa Tambwe.
Msimu
uliopita, Yanga walipoteza dira ya kutwaa ubingwa kufuatia kuchapwa 2-1
na Mgambo katika uwanja huu wa Mkwakwani, lakini jana wamelipa kisasi.
Mgambo waliwafunga Simba 2-0 jumatano ya wiki hii, lakini jana mambo yaliwageukia kwa kula kichapo kama hicho. |
No comments:
Post a Comment