DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 19, 2015

MAN CITY CHALI UEFA

Barcelona wakishangilia bao lao lililofungwa na Ivan Rakitic dakika ya 31.
Barcelona imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Manchester City bao 1-0 lililofungwa na Ivan Rakitic dakika ya 31 ya mchezo uliopigwa Nou Camp, Barcelona usiku huu na kuitupa nje City kwa jumla ya mabao 3-1.
Patashika wakati wa mtanange huo uliopigwa Nou Camp, Barcelona.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, straika wa Juventus, Carlos Tevez aliifungia timu yake mabao 2 dakika ya 3 na 79 wakati ikiichapa Borussia Dortmund kwa mabao 3-0 huku bao lingine likiwekwa kimiani na Alvaro Morata dakika ya 70.
Manchester City vichwa chini baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo. Katika mechi ya kwanza iliyopigwa Etihad nchini England, Manchester City walilala kwa mabao 2-1.Kwa matokeo hayo, Juventus nao wamefuzu hatua ya robo fainali huku Dortmund wakifunga virago. CHANZO. MJENGWABLOG.

No comments:

Post a Comment