Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja kesho
tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi
la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa
vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka
1990, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015
kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo
Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.
Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa
Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu
Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa
Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza
157.
Imetolewa na;
Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.
|
No comments:
Post a Comment