Mbunge wa Jimbo la Kigoma
Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Kabwe Zubeir
Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
huenda muda si mrefu kuanzia sasa akalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano
ikiwa ni Hotuba ya kuaga na kung’atuka kushika wadhifa huo wa uwakilishi wa
wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Zitto ni Mchumi wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam aliingia Bungeni kwa mara ya Kwanza mwaka 2005 akiwakilisha
wananchi wa Kigoma Kaskazini kupitia chama cha Chadema.
Ameamua kuachia wadhifa huo na
huenda pamoja na uanachama wake wa Chadema kufuatia mgogoro wa kisiasa uliopo
baina yake na uongozi wa Chadema.
Machi
15 Kabwe Zitto aliwaaga wapiga kura wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kuwa
hatokuwa tena Mbunge wao baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
“Ni
wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti
pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia”…”Sitakuwa
mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea
maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine”.
Zitto
amekuwa Mwanachama wa Chadema kwa takribani miaka 24 ambapo akiwa amejiunga
angali bado kijana mdogo na alifanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali katika
chama hadi Naibu Katibu Mkuu Bara.
|
No comments:
Post a Comment