MASHEIKH
wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi
kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais
2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia) na Alli Mtumwa
(wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na
kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.
Mashekhe
hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika
salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye
(Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na
wapo nyuma yake katika dua.
Lowassa
amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii
yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike
sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila
nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku
ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu,"alisema.
Lowassa
amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha
anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za Elimu,
afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.
| |
No comments:
Post a Comment