Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe, akizungumzia moja ya vipengele vipya vilivyofanyiwa maboresho kwenye tuzo hizo. |
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikoli, akielezea namna ya mchakato wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka huu jinsi zitakavyofanyika. |
Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, akizungumzia jinsi baraza hilo lilivyoboresha baadhi ya vitu kwenye tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu. |
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini baadhi ya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye kikao cha uzinduzi huo.
MUDA wa
utoaji tuzo kwa wasanii wa Tanzania wanaofanya vizuri umewadia na tayari
mchakato wa awali wa mchanganuo wa tuzo hizo zinazojulikana kama Kili
Tanzania Music Awards 2015 (KTMA) umetangazwa rasmi leo.
Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, ambao ndiyo wadhamamini wakuu wa
tuzo hizo kupitia usimamizi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA),
aliweka wazi kuhusiana na mchakato mzima wa mwaka huu utakavyokuwa
kwenye hafla fupi iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa LAPF uliopo
Kijitonyama, Dar es Salaam.
Kikuli
alifafanua kuwa kuna vitu vingi vimeongezeka katika msimu, huu lengo
likiwa ni kuboresha utoaji na zoezi zima la tuzo hizo. Mojawapo ni
kuwapa fursa Watanzania kupendekeza wasanii watakaowania tuzo hizo kwa
kuwapigia kura waingie kwenye kinyang’anyiro kwa njia tatu kuu.
“Tumekuwa
na juhudi za makusudi za kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa
wataalam mbalimbali kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na
kuziongezea thamani tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu
kuongezeka kwenye medani za kimataifa.
“Wananchi
watapata fursa ya kupiga kura kupendekeza wasanii katika vipengele
mbalimbali kwa kutumia njia tatu; kwa mfumo wa Website ya www.ktma.co.tz, mfumo wa mtandao wa WhatsApp na kwa njia ya SMS pia,” alisema Kikuli.
Aidha,
katika mfumo mpya wa WhatsApp mpiga kura ataweza kutumia namba ya 0686
528 813 na SMS pia kutumia namba 15415 kwa kutuma ujumbe wa neno KTMA au
KILI na kisha kufuata maelekezo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo
litaloanza rasmi Machi 30 mpaka Aprili 19, mwaka huu litakapositishwa.
Baada ya
upigaji wa kura hizo kutakuwa pia na michakato mingine itakayofuata
katika kuwatafuta washindi mpaka mwisho wa utoaji wa tuzo hizo kama
kuchuja wapendekezwa kabla ya kuwarudisha tena kwa wananchi na kupigiwa
kura za ushindi kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL).
|
No comments:
Post a Comment