Mwimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injili nchini, Jennifer Mgendi, ameachia albamu yake mpya mapema wiki hii.
Akizungumza
na blogu hii Mgendi amesema albamu hiyo ina jumla ya nyimbo saba ambazo
ni Wema ni Akiba, Nani kama Mungu?, Nakungoja aliomshirikisha Mchungaji
Abiudi Misholi, Kimbilia Msalabani, Nakuhitaji Roho, Tenda nishangae na
Wastahili.
Akizungumzia
video ya albamu hiyo, Mgendi amesema maandalizi ya video yameanza na
video itazinduliwa rasmi Juni 28 katika kanisa la DCT Tabata Shule katika
tamasha litakaloambatana na shukurani ya kutimiza miaka 20 tangu aanze
uimbaji.
Mbali na
uimbaji Jennifer pia ni muandaaji na mwigizaji wa filamu mbalimbali za kidini hadi
sasa akiwa na filamu tano Joto la roho, Pigo la faraja, Teke la Mama,
Chaimoto na Mama Mkwe. |
No comments:
Post a Comment