DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Wednesday, March 25, 2015

VIONGOZI WA DARUSO WATINGA BUNGENI DODOMA

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) leo wametinga Bungeni katika ziara ya kimafunzo na kupokelewa na Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Dk Fenela Mukangara. Wakiwa Bungeni viongozi hao ambao ni Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri na Wabunge walijionea namna shughuli za Bunge zinavyoebndeshwa chini ya Spika Anna Makinda.
 Mmoja wa viongozi hao akifuatilia kwa umakini shughuli hizo za bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma katika Mkutano wake wa kumi na tisa (19) Kikao cha nane.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Febela Mukangara katika picha ya pamoja.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Febela Mukangara akipiga nao picha. Vijana hao walifika Bungeni kwa Mualiko wake.
 

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Febela Mukangara akiwa na wageni wake.

No comments:

Post a Comment