Na Kibada Ernest Kibada -Sumbawanga
………………………………………..
AFISA Misitu wa Wakala wa Misitu
mkoani Rukwa , Victoria Kamage (29) na dereva wake wamekufa papo
hapo na kujeruhiwa watu wengine watatu kujeruhiwa kufuatia magari
mawili kugongana uso kwa uso katikati ya daraja la Lwichwe , Manispaa
ya Sumbawanga katika barabara kuu ya Sumbawanga – Namanyere – Mpanda .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda
akitthibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha Land Cruiser
yenye nambari za usajiri EFP 7307 mali ya Wakala wa Misitu (TFS) na
gari kubwa aina ya Scania yenye namba za usajiri T 748 ABF mali ya
Seleman Kapilimka .
Kwa mujibu wa kamanda Mwaruanda ajali hiyo ilittokea saa
nne usiku jana kwa kugongana uso kwa uso ambapo dereva wa gari dogo
aina Land Cruiser aitwae Sizya Mhagama alifikwa na umauti wakati
akipata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga .
Gari hilo la Land Cruiser kwa mujibu wa kamanda Mwaruanda
likuwa na abiria watano ambapo watatu wakiwemo Ofisa Maliasili ,
Venance Mwambo (23) na watoza ushuru wa mazao ya misitu wa wakala wa
misitu waliotambuliwa kwa jina moja moja ya Wilson na Macha .
Aliongeza kuwa amjeruhi hao hali zao ni tete ambapo
wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa kwa matibabu
katika chumba maalumu cha ungalizi (ICU).
Kamanda Mwaruanda alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa gari hilo dogo ambalo lilikuwa likifuatilia gari
lingine lililokuwa na shehena ya mkaa likitokea wilayani Nkasi
baada ya kupewa taarifa ya gari hilo .
Aliongeza kuwa dereva wa Scania aitwae Jofrey Luhanga (32)
anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa mahojiano ambapo
atafikishwa mahakamani muda wowote baada ya upelelezi wa awali wa
shauri lake kukamilika.
|
No comments:
Post a Comment