Aliyekuwa mchezaji wa
timu ya Taifa ya Brazil Legend Pele ametamka bayana kwamba Messi ni bora
kuliko Ronaldo na bora zaidi duniani.
Mchezaji huyo kutoka
timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya soka ya Barcelona kutoka Hispania
alijinyakulia tunzo 4 za mchezaji bora wa dunia ukilinganisha na
Ronaldo ambaye anazo 3 akiwa anaitunikia Real Madrid na timu yake ya
Taifa Ureno.
Pele alisema ” wakati
mwingi sana watu wamekuwa wakilinganisha ubora wa Messi na Ronaldo
lakini wana aina tofauti ya mchezaji, alisema mchezaji huyo ambaye
alifanikiwa kushinda kombe la dunia Mara 3 akiwa na timu yake ya Brazil.
Pele alizidi kusesema “Ni wachezaji wawili wakubwa lakini kwa miaka 10 iliyopita Messi amekuwa bora.
|
No comments:
Post a Comment