DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 19, 2015

KAMPUNI YA ACACIA YATOA TUZO KWA WAFANYAKAZI WAKE

Meneja wa usalama na operesheni wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (mstaafu), Abdallah Mssika, (katikati), akipokea tuzo ya umahiri ya ‘cacia CEO Excellence Award 2014’ na Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Brad Gordon, wakati wa hafla ya kutoa tuzo kwa viongozi wa juu wa mgodi na wafanyakazi waliofanya vizuri mwaka uliopita. Hafla hiyoilifanbyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu, wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga juzi. Kushoto ni Meneja wa mgodi wa Bulyanhulu, Michel Ash.
Meneja wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, Michel Ash, (kushoto), akimkabidhi tuzo ya umahiri ya Acacia CEO Excellence Award 2014, mfanyakazi wa mgodi huo, Andy Mwakibete, wakati wa hafla ya kutoa tuzo iliyofanyika kwenye mgodi huo juzi.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), akimkabidhi tuzo ya umahiri 'CEO Excellence Award', afisa kutoka kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa umma wa mgodi wa dhahabu wa North Mara, Geoffrey Nangai, aliyepokea kwa niaba ya mgodi huo, kwenye hafla ya kila mwaka ya kutoa tuzo kwa vitengo na wafanyakazi mmoja mmoja wa kampuni ya Acacia ilifanyika juzi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, wilaya ya Msalala mkoa 2wa Shinyanga.
Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Michel Ash, akitoa hotuba.
 Afisa Mtedaji Mkuu wa Acacia, Brad Gordon, akitoa hotuba.
Wafanyakazi wa Acacia, wakisikiliza hotuba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon.
Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, akiserebuka wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment