DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Thursday, March 19, 2015

ZIARA YA LUKUVI LONGIDO, ARUSHA

Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana.
Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Msafara wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ukiingia eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zilijengwa na NHC Wilayani Longido ili kufungua rasmi nyumba hizo baada ya kukamilika ujenzi wake.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea kwa furaha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC ili kufanya ufunguzi rasmi.
Wafanyakazi wa NHC nao hawakuwa nyuma kumpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili mradi wa NHC Longido kufanya ufunguzi rasmi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akifungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba na kuingia ndani kukagua nyumba hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa Wilayani Longido.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda akilishukuru Shirika la Nyumba kwa kujengwa nyumba Wilayani Longido eneo ambalo ni kame na lenye changamoto kubwa ya kutekeleza ujenzi wa nyumba bora.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya wananchi wa Longido (hawapo pichani)waliohudhuria ufunguzi alioufanya wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Levolosi Jijini Arusha.Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment