Mbunge
wa jimbo la Monduli Mkoani Arusha na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa
akizungumza na kundi la makada wa chama cha Mapinduzi na waendesha
Bodaboda kutoka Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya waliotembelea nyumbani
kwake mjini Dodoma hii leo kumtaka asiache kuchukua fomu ya kugombea
Urais mwaka 2015 maana yeye ndio chaguo lake.
Aidha
Lowassa ametoa rai kwa watu wengine mbalimbali katika jamii ambao
huenda wana nia au mpango wa kuja kwake kusitisha kufanya hivyo na
kusibiri chama kitakapotoa maelekezo kwani kwa sasa yeye atashijndwa
kuzuia.
"Utaratibu
huu ulioanzwa na watu mimi ni vigumu kuuzuia mafuriko kwa mikono,
mafuriko yanakuja mimi nizuie kwa mikono ntaweza kweli? hawa watu sina
hoja nao sina cha kuwaambia ila nashauri tufanye hivii, wengine ambao
hawajaja hebu tusubiri chama kitoe maelekezo.
Lowassa
amesema kuwa watu wanavyo fanya inatafsiriwa kama ni kampeni inagawaje
Rais alikwisha kusema mjini Songea kuwa mkiona hawa hawatoshi shawishini
wengine.
|
No comments:
Post a Comment