DOM LAND BLOG

DOM LAND BLOG

Sunday, March 22, 2015

ENRIQUE:EL CLASSICO HAIWEZI KUAMUA MSHINDI

Kocha wa Barcelona Luis Enrique.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa mchuano wa Jumapili (leo) kati ya wapinzani wakuu katika ligi ya La Liga, Real Madrid na Barcelona haitaamua ni nani atakayeshinda ligi.
Huku ikiwa takriban mechi 11 zimechezwa, kilabu ya Barcelona iko mbele na pointi moja dhidi ya Real Madrid.
Messi na Ronaldo
''Ni mechi muhimu lakini sio itakayotoa mshindi wa ligi, alisema Enrique ambaye aliwahi kuzichezea timu zote mbili. Mechi hizi huwa tofauti sana ukilinganisha na nyengine,ni mahasimu wetu wa jadi. Pia, kuna tofauti ya mabao yaliyofungwa kati ya timu hizi mbili. Hakuna mshindi wa moja kwa moja anayepigiwa upato wakati wa mechi kama hizi, lakini tunapocheza mbele ya mashabiki wetu sisi hupata motisha zaidi''.alijigamba Luis Enrique.
''Hii ni fursa nzuri ya kuongeza pengo dogo lililopo kati yetu na Real Madrid''. Aliongezea kocha huyo. BBC.

No comments:

Post a Comment