Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu
ASASI
ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya
kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya
matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea
kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya
albino.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa
Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu amesema
matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu
kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji
ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015.
Alisema
matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo
yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu
ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo
kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za
kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema 'Imetosha Mauaji ya
Albino'.
"...Baada
ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi
kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo,
karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali
wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu," alisema Mdimu katika
taarifa yake.
Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai
kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi
au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa
kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo.
"...Hili
suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu
za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo
tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu
kuahirishwa.
"Tulikuwa
tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha...sasa
imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. Napenda
kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na
kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu,"
Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni
kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa
mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa
watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi.
|
No comments:
Post a Comment